Zenj FM

Airpay Tanzania kuwa mkombozi wa uchakavu wa noti nchini

25 October 2023, 5:26 pm

Mwanzilishi wa Airpay Tanzania Yasmini Chila akizungumza katika uzinduzi wa taasisi hiyo. Picha na Mary Julius.

Na Mary Julius.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum  amesema kuzinduliwa kwa mfumo wa kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa Airpay Tanzania utaisadia noti za Tanzania kuwa katika mzunguko kwa muda mrefu.

Waziri Saada  ameyasema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi  katika uzinduzi wa Airpay Tanzania uliofanyika hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege.

Amesema Airpay itaweza kusaidia kupunguza matumizi ya malipo taslimu sokoni na badala yake kutumia mtandao ambapo utasaidia kuiwezesha fedha kutokuchakaa na kuingiza serikali hasara ya kuzalisha fedha mpya kila mara.

 Aidha amesema mfumo huo utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kutumia mfumo wa kidigital wa kufanya malipo pamoja na kuongeza usalama wa fedha.

Sauti ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya .

Kwa upande wake mwanzilishi wa  Airpay Tanzania Yasmin Chali amesema  mfumo huu utaweza kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo  visiwani Zanzibar katika kufanya malipo kwa njia ya matandao

Aidha amesema Airpay Tanzania inatarajia kuanzisha chuo kwa ajili ya kutoa elimu kwa  wajasiliamali ili waweze kutumia mifumo ya fedha ya kidigital.

Sauti ya mwanzilishi wa Airpay Tanzania Yasmin Chali.

Kwa upande wake Waziri  Nchi Ofisi ya Raisi Kazi Uchumi na Uwezeshaji Mudrik Ramadhan Soraga amesema mfumo huu utasaidia serikali ya mapinduzi ya zanzibar  kuwa na takwimu sahihi za wajasiriamali walio sajiliwa pamoja na kujua  idadi ya wajasiriamali ambao  wanalipa kodi.  

Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mudrik Ramadhan Soraga