Zenj FM

Mrajis Zanzibar awakumbusha SHIJUWAZA kuchagua viongozi bora

15 April 2024, 4:37 pm

Mrajisi Asasi za Kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla (aliye simama) akifungua mkutano wa pili wa uchaguzi wa shirikisho la SHIJUWAZA.

Na Mary Julius.

Shirikisho la Jumuiya za watu wenye ulemavu limesajiliwa rasmi mwaka 2014 mpaka sasa  linawanachama 12.

Mrajisi Asasi za Kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla amewataka  viongozi wa shirikisho la jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) watakao chaguliwa  kuziunganisha jumuiya zilizo chini yao.

Mrajisi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi  ulio fanyika katika ukumbi UWZ Kikwajuni Zanzibar  amesema Kuna baadhi ya jumuiya zinajiona kuwa ni wakubwa kuliko shirikisho hilo  hivyo ni wajibu wa viongozi watakao chaguliwa kuwaunganisha na kuwa kitukimoja ili kuleta maendeleo  kwa wanajumuiya.

Aidha amewataka wapiga kura kuwachagua viongozi Bora  watakao wavusha vyema kwa kipindi Cha miaka minne.

Sauti ya Mrajisi Asasi za Kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla

Akizungumza katika uchaguzi huo katibu mkuu wa zamani SHIJUWAZA Juma Salim Ali amesema shirikisho hilo katika kipindi Cha miaka nne limeweza kupata ufadhili wa sh billion 1 milioni 157 laki tano thelethini na tano elfu.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Zamani SHIJUWAZA Juma Salim Ali.

Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Shirikisho la shijuwaza Ali Omary Makame  aliyepita kwa kuchaguliwa kwa kura Za ndio kwa asilimia 89 amesema wamekusudia kujipanga na kuhakikisha wanasimamia haki na fursa za watu wenye ulemavu.

Sauti ya Makamo Mwenyekiti wa Shirikisho la shijuwaza Ali Omary Makame

Walio chaguliwa katika uchaguzi huo  ni pamoja na Mwenyekiti Mwanadawa Khamis Mohamme, Makamo Mwenyekiti ni Ali Omari Makame,Katibu  Mkuu ni Tifly Mustafa Nahoda wengine ni Naibu Katibu kuu, Jide Khamis Swaleh,