Zenj FM

Airpay Tanzania yaleta neema kwa wajasriamali Zanzibar

21 September 2023, 2:25 pm

Mwanzilishi wa kampuni ya Airpay Tanzania Kunal Jhunjhunwala Ckatikati) na Mwanzilishi Mwenza wa Airpay Tanzania, Yasmin Chali wakiwa pamoja na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga aliyevaa suti Nyeusi.

Na Mary Julius.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga  amesema ujio wa kampuni ya Airpay  Tanzania, Zanzibar itasaidia  serikali  kuwafikia wajasiriamali wadogo katika kupata fursa za mikopo na kutambulika.

Soraga ameyasema hayo wakati akifungua  ofisi ya kampuni  ya Airpay Tanzania katika jengo la Muzamir Mlandege Zanzibar, amesema AIRPAY itawezesha wajasiriamali kujisajil na kuweza kutambulika  kupata huduma za fedha kidigital.

Aidha  amesema kampuni hiyo ambayo ni ya kwanza kuwa na makao makuu Zanzibar  itasaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika ukusanyaji wa Kodi .

Sauti ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga

Akizungumza katika uziinduzi huo Makamu Rais na Meneja Mikakati Wa Kampuni ya Airpay Tanzania  Mihayo Wilmore  amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha inawafikia  wajasiriamli wadogo na kuwaingiza katika mfumo wa air pay ambao utawezesha wafanyabiashara wa aina zote kutumia

Aidha amesema mfumo wa AIRPAY utasaidia wajasiriamali kuweza kukopeshwa na  mabenki kwani taarifa zao za siku mwezi mpaka mwaka zitaonekana katika mfumo huo Hali amabayo itamsaidia mjasriamali kutunza kumbukumbu zao za biashara. 

Sauti ya Makamu Rais na Meneja Mikakati Wa Kampuni ya Airpay Tanzania  Mihayo Wilmore

 Kwa upande wake Meneja Uchumi wa Banki Kuu ya Tanzania Ofisi ya Zanzibar Moto Ngwinganele Lugobi  amesema bot imejiridhisha kuwa AIRPAY inauwezo wa kufanya huduma za kifedha na ndio maana wamewapatia leseni ya kufanya hivyo .

Sauti ya Meneja Uchumi wa Banki Kuu ya Tanzania Ofisi ya Zanzibar Moto Ngwinganele Lugobi

 Kampuni ya Airpay ina uzoefu wa muda wa miaka 12 na makao yake makuu ni nchini India