Zenj FM

Kusini Pemba kupambana na vifo vya mama na mtoto

17 September 2026, 21:50

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Zuhura Mgeni Othman akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika kikao kazi cha kuimarisha utoaji wa huduma Bora ikiwa ni miongoni mwa mkakati wa kupunguza vifo vya mama na mtoto

Madaktari na watoa huduma za afya Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kuwajibika katika kutoa huduma bora kwa mama wajawazito ili kupunguza vifo vya mama na mtoto. Viongozi wa afya wamesema kupunguza vifo hivyo ni jukumu la kila mmoja, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau. Shirika la PharmAccess limewataka wadau kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za pamoja katika kuondosha kabisa vifo vya mama na mtoto.

Na Is haka Mohammed.

Madakari na watoa huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya katika Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kuwajibika wanapotoa huduma kwa mama wajawazito ili kufikia lengo la kupunguza na kuodosha kabisa vifo vya mama na mtoto kwenye mkoa huo.

Wito huo umetolewa na Mkuu Wilaya ya Chake Chake Zuhura Mgeni Othman wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid kwenye kikao kazi cha kuimarisha ubora wa huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na mtoto  katika mkoa huo.

Sauti ya Mkuu Wilaya ya Chake Chake Zuhura Mgeni Othman

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Zanzibar ni jukumu la kila mmoja.

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji

Mwakilishi wa Shirika Pharm Access  Leberata Shijja ametoa wito kwa wadau kushirikiana katika kupunguza na kuondosha kabisa vifo vya mama na mtoto.

Sauti ya Mwakilishi wa Shirika Pharm Access  Leberata Shijja,