Zenj FM

Manispaa Kati yahamasisha ulipaji kodi kwa maendeleo

19 April 2026, 5:19 pm

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Daktari Mwanaisha Ali Said akitoa ufafanuzi wa taarifa ya bajeti ya makadirio, makusanyo na matumizi ya fedha kwa mwaka 2026/2027 katika kikao cha Bajeti cha Baraza la Manispaa hiyo. Huko katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Baraza la Manispaa Kati limepanga kukusanya jumla ya shilingi bilioni 2.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya milioni 400 kutoka mwaka uliopita. Mkurugenzi Dk. Mwanaisha Ali Said amesema ongezeko hilo litatokana na kuboresha ukusanyaji na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato.

Na. Hakika Mwinyi

Baraza la Manispaa Kati limepanga kukusanya Jumla ya Shilingi Billioni 2.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali Said katika kikao cha Bajeti ya Baraza hilo hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga.

Amesema kunaongezeko la zaidi ya millioni Mia Nne ambayo wamepanga kukusanya katika mwaka mpya wa fedha  pamoja na kuongeza vyanzo vipya vya mapato ndani ya baraza hilo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali Said.

‎Akitoa ufafanuzi kuhusiana na bajeti hiyo Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban ameeleza kuwa bajeti hiyo imejikita katika maeneo matatu ambapo asilimia 10 itakwenda kwa vijana, kinamama pamoja na watu wenye Mahitaji malum.

Aidha Meya huyo amewaomba wananchi wa Wilaya hiyo kulipa kodi kwa wakati ili kufikia malengo waliojiekea ya kuimarisha miradi ya Maendeleo ndani ya wilaya hiyo.

Sauti ya Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban.