Zenj FM

ZAWEMA waeleza umuhimu wa vipimo katika maendeleo ya Zanzibar

16 May 2026, 22:15

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar,ZAWEMA Mohamed Mwalimu Simai akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ZAWEMA  zilizopo Malindi, Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Weights and Measures Agency, Mohamed Mwalimu Simai, ametoa wito kwa jamii kuelewa matumizi sahihi ya vipimo katika biashara ili kujilinda dhidi ya udanganyifu. Amesema sayansi ya vipimo ina mchango mkubwa katika kujenga uaminifu kwenye biashara, uandaaji wa sera na kulinda haki za watumiaji pamoja na wafanyabiashara.

Na Mary Julius.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar,ZAWEMA Mohammed Mwalimu Simai, ametoa wito kwa jamii kuwa na uelewa wa vipimo vinavyotumika katika biashara ili kujilinda dhidi ya udanganyifu na hasara zinazoweza kujitokeza katika miamala ya kila siku.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ZAWEMA  zilizopo Malindi, Zanzibar, kuelekea maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Mei 20, amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara kutofahamu matumizi sahihi ya vipimo huku wengine wakiongeza vipimo kupita kiwango kwa lengo la kuwaridhisha wateja wao jambo ambalo pia halikubaliki kisheria.

Sauti Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar,ZAWEMA Mohammed Mwalimu Simai.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Sayansi ya Vipimo Inajenga Uaminifu Katika Uandaaji wa Sera” inalenga kuonesha umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na tathmini ya sera zinazotekelezwa.

Aidha amesema wakati wa kuandaa sera ni muhimu kutumia vipimo sahihi katika kufanya tathmini ya utekelezaji wake ili kubaini kiwango cha mafanikio kilichofikiwa katika sekta mbalimbali.

Sauti Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar,ZAWEMA Mohammed Mwalimu Simai.

Mkurugenzi Mohammed  amesema katika kuelekea maadhimisho hayo, wakala huo unatarajia kufanya ukaguzi wa mizani na vipimo vinavyotumika katika hospitali kwa ajili ya kupima wagonjwa huku akieleza kuwa kila sekta hutumia aina tofauti za vipimo kulingana na mahitaji yake.

Sauti Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar,ZAWEMA Mohammed Mwalimu Simai.

.Aidha Mkurugenzi Mohammed  ameeleza kuwa Zanzibar inategemea bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi, hivyo ZAWEMA umeanza kufanya ukaguzi wa bidhaa za ujenzi kama saruji na nondo ili kuhakikisha zinakidhi viwango rasmi.