Zenj FM
Zenj FM
9 September 2025, 7:53 pm

Na Mary Julius
Wagombea watano wa nafasi ya Urais wa Zanzibar wamerejesha fomu zao kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilisha masharti yote ya kisheria, ikiwemo kupata wadhamini wasiopungua 1,000 kutoka katika mikoa yote mitano ya Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake Mgombea wa Chama cha MAKINI, Ameir Hassan Ameir, ameahidi kufuata nyayo za Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Mzee Abeid Amani Karume, kwa kuhakikisha analeta maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.
Kwa upande wake, Mgombea wa chama cha ADA-TADEA, Juma Ali Khatib, amesisitiza kuwa uamuzi wa chama chake kumuunga mkono Mgombea wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, si wa mtu binafsi bali ni azimio la pamoja la chama.
Hadi sasa, wagombea watano kati ya 17 waliopanga kugombea wamesharejesha fomu kwa ZEC.