Zenj FM

Zanzibar watakiwa kuchangia damu

7 May 2024, 5:41 pm

Baadhi ya wananchi wakichangia damu katika eneo la Mapinduzi Squre Kisonge.

Ukosefu wa damu ni moja ya sababu inayosababisha vifo vya mama na mtoto Zanzibar.

Na Mary Julius

Wananchi wametakiwa kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao wanahitaji huduma hiyo katika hospitali za Unguja na Pemba.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Habiba Hassan Omar katika bonanza la uchangiaji damu katika viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge.

Amesema Zanzibar inahitaji unit za damu elfu 13 kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuweza kusaidia watu wenye mahitaji jambo ambalo kwa sasa limekuwa halifikiwi na kusababisha upungufu wa damu katika hospitali za serikali na binafsi.

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Habiba Hassan Omar.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Wauguzi na Wakunga Mwanaisha Juma Fakii amesema ukosefu wa damu ni moja ya sababu inayosababisha vifo vya mama na mtoto Zanzibar.

Amesema vifo vya mama na mtoto vimekuwa vikiongezeka Kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa damu hivyo ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Sauti ya Mkurugenzi Idara ya Wauguzi na Wakunga Mwanaisha Juma Fakii

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu wamewaomba wananchi kupenda kuchangia damu ili kusaidia watu wenye mahitaji damu.

Sauti mwananchi

 Bonanza la uchangiaji damu limeandaliwa na Jumuiya ya Wauguzi kwa kushirikiana na Milele Foundation.