Zenj FM

Vijana Pemba waomba ajira ujenzi uwanja wa ndege

24 September 2023, 3:08 pm

Mawaziri wa Serikali ya SMZ Dkt. Khalid Salim Moh`d, ( kati )Hamza Hassan Juma na Dkt. Saada Mkuya Salim wakiwa kwenye mkutano na wananchi wa vijiji vya Furaha, Mvumoni na Mfikiwa wilaya ya Chake ambao wanatarajiwa kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba.
 

Wananchi waliopisha ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba kuanza kulipwa fidia mara baada ya kukamilika kwa tathmini.

Na Is-haka Mohammed

Kamati ya  muda ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  inayoratibu  masuala ya ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba imekutana na wananchi  wa vijiji vya Furaha, Mvumoni na Mfikiwa ambao watahamishwa kwenye maeneo hayo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa kujadiliana  juu ya malipo ya fidia yanayotegemewa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza na wananchi hao Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri hao ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salim Moh`d amesema  tayari ripoti ya mthamini kuu imeshakamilishwa na kukabidhiwa wizara hiyo na hivi punde itakabidhiwa kwa wizara ya fedha ni shughuli za ulipaji zianze.

Sauti ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salim Moh`d.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salim amewahakikishiwa wananchi hao kuwa fedha kwa ajili ya fidia kwa wananchi hao zipo kilichokuwa kikisubiriwa na ripoti ya mtathmini na muda wowote zoezi la ulipaji litaanza kufanyika.

Sauti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salim.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud amewapongeza wananchi hao kwa uvumilivu mkubwa waliouonyesha kwa serikali na kuwataka kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kifupi kilichosalia.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud.

Kwa upande wao wananchi wa maeneo hayo ambayo ni Furaha, Mvumoni na Mfikiwa wameomba wakati wa utekelezaji wa mradi vijana wao wasiachwe watakapohitaji wafanyakazi wakati wa ujenzi.

Sauti ya Mwananchi.