Zenj FM

Wito kwa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto

16 June 2026, 21:24

Mkuu wa Divisheni ya Mapato, Uchumi na Wajasiriamali Baraza la Manispaa Kati Mussa Abdurab Fadhil akizungumaz katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Wazazi na walezi wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kushiriki kikamilifu katika kuwafundisha kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuimarisha elimu yao. Wito huo umetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, ambapo imeelezwa kuwa malezi na elimu ya mtoto ni jukumu la pamoja kati ya wazazi na walimu.

Na Hakika Mwinyi.

Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya Watoto wao pamoja na kuwafundisha  kuweza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.

 Mkuu wa Divisheni ya Mapato, Uchumi na Wajasiriamali Baraza la Manispaa Kati Mussa Abdurab Fadhil ameyasema hayo katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Amesema jukumu la kuwafunza  Watoto sio la Walimu pekee kwani hata Mzazi anawajibu wakumfundisha Mtoto kuhakikisha anajua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu nambari.

Sauti ya Mkuu wa Divisheni ya Mapato, Uchumi na Wajasiriamali Baraza la Manispaa Kati Mussa Abdurab Fadhi

Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya ya Kati Somoe Said Mussa amesema Mtoto anahaki mbalimbali katika jamii ambazo anahitaji kupatiwa ikiwemo Kulindwa, Kuthaminiwa pamoja na kupatiwa elimu bila ya ubaguzi wowote.

Sauti ya Afisa Elimu Wilaya ya Kati Somoe Said Mussa

Nae Mwalimu wa Skuli ya Maandalizi Binguni Khadija Mshimba Makame amewaomba Wazazi kuwa karibu na Watoto wao hususani wanaporudi nyumbani ili kuepukana na  udhalilishaji wa kijinsia.

Sauti ya Mwalimu wa Skuli ya Maandalizi Binguni Khadija Mshimba Makame

Jumla ya Skuli kumi 10 za Maandalizi Wilayani humo zimeshiriki katika ‎Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afirika ambayo huadhimishwa kila ifikapo  Tarehe 16 mwezi 6 kila mwaka na kauli mbiyu ya mwaka huu inasema Linda Mtoto wa Afrika, Afya bora na Maisha bila ya udhalilishaji.