Zenj FM
Zenj FM
27 July 2026, 15:17

Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeshauriwa kuanzisha kampasi Kisiwani Pemba ili kuongeza fursa za elimu ya juu na kurahisisha upatikanaji wa kozi kwa vijana wa eneo hilo bila kulazimika kwenda nje ya Pemba. Aidha, viongozi na wawakilishi wa vyuo wamewahimiza wanafunzi kutumia fursa za masomo zinazotolewa na taasisi mbalimbali, huku TIA ikisisitiza maadili bora na mazingira salama ya kujifunzia.
Na Is haka Mohammed.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeshauriwa kuanzisha Kampass ya Chuo hicho Kisiwani Pemba ili kutanua wigo na kuwarahishia vijana na wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari na wanao uhitaji wa kusomo fani zinazotolewa na taasisi kuzipata kisiwani hapo badala ya kuzifuata nje ya Pemba.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo huko Gombani Chake Chake Pemba katika Wiki ya Maonyesho ya Vyuo Vya Elimu ya Juu lililoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar(WEMA).
Aidha D.C Ali amewataka wawakilishi wa Taasisi hiyo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa vijana katika maeneo tofauti ili vijana hao wawe na uanda mpana wa kuchaguzi kozi za kujiendeleza pamoja na kusifia sifa za utoaji wa elimu katika taasisi hiyo.
Mapema Afisa Udahili wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Adamu Mtego amewatoa hofu wazazi na walezi kuwasomesha watoto katika vyuo vilivyopo Tanzania bara kwani Chuo hicho kinazingatia misingi ya maadili na malezi.
Kwa upande nao baadhi ya wawakilishi wa vyuo mbali mbali kaika maoneysho hayo akiwemo Mgeni Ali kutoka Chuo Kikuu Cha Kampala amewataka wanafunzi walimaliza fom six ambao hawakupata ufaulu mzuri kutokata tamaa na badala yake kujiunga na chuo hicho kuendeleaza masomo yao.
Amesema chuo hicho ambacho kinatoa Udahili wa kozi kina fursa ya kipekee kwa watuo wanaofanyakazi kwa kuweza kusoma kupitia Programme maalum inayowawezesha kwe kusoma kupitia Online huku wakishiriki masomo ya pamoja katika mwezi wa sita na mwezi wa 12 kwa kila mwaka.