Zenj FM

Serikali yaongeza juhudi kupunguza vifo vya mama na mtoto

21 September 2026, 13:12

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya akizungumza katika Ukumbi wa Utaani Wete wakati akifungua Kikao Kazi cha Kuimarisha Huduma za Afya na Kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya ametoa wito kwa kila mmoja kushiriki katika juhudi za kupunguza vifo vya mama na mtoto, akisisitiza kuwa ni jukumu la pamoja.

Na Is-haka Mohammed.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya amesema Kampeni ya kupunguza vifo vya mama na mtoto ni jukumu na kila mmoja kuweza kushiriki kulingana nafasi yake popote pale alipo.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Utaani Wete wakati akifungua Kikao Kazi cha Kuimarisha Huduma za Afya na Kupunguza vifo vya mama na mtoto katika Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwashirikisha wadau mbali mbali.

Amesema juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto hazitozaa matunda kama kila mtu hakutimiza wajibu wake.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema uwekezaji mikubwa uliofanya na Serikali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita zimeanza kuzaa matunda katika kuimarisha Afya ya mama na mtoto na kupunguza kwa kiasi vifo vya mama na mtoto.

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mngereza Mzee Miraji

Meneja wa Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Zanzibar Dkt. Kamiliya Ali Omar amesema suala na ufuatiliaji ni muhimu katika kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini.

Sauti ya Meneja wa Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Zanzibar Dkt. Kamiliya Ali Omar