Zenj FM

Viongozi jimbo la Amani  waungana kuwainua vijana wa gereji na bodaboda

2 November 2026, 16:19

Mbunge wa Jimbo la Amani Abdul Yussuf Maalim na Mwakilishi wa jimbo hilo Masoud Amour Masoud, wakikabidhi spana kwa fundi mkuu wa gereji ya Kwawazee Frank Wiliam .

Mbunge Abdul Yussuf Maalim na Mwakilishi Masoud Amour Masoud waungana kuwainua vijana wa gereji na bodaboda Jimbo la Amani kwa kuwakabidhi vifaa vya kazi. Viongozi hao wawataka vijana kudumisha amani, kujiajiri na kujiepusha na vitendo visivyofaa kwa maendeleo yao na jamii.

Na M

Vijana wametakiwa kudumisha amani, kuachana na vitendo visivyofaa, kujikita katika shughuli halali za kujipatia kipato, ikiwemo ufundi na biashara, ili kujenga maisha yao na kuchangia maendeleo ya jamii.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Amani, Abdul Yussuf Maalim, wakati wa ziara yake kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Jimbo hilo, Masoud Amour Masoud, walipotembelea gereji mbalimbali na kuwakabidhi vijana vifaa vya kazi vikiwemo spana, pamoja na vikoti vya kujikinga na upepo kwa waendesha bodaboda.

Maalim amesema ziara hiyo ni sehemu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwao, ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi, kutambua changamoto zao na kusaidia kupunguza makali ya maisha.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Amani, Abdul Yussuf Maalim.

Akizungumzia mvua za El Niño Mbunge amewataka vijana kushiriki usafi wa mazingira na kusafisha mitaro ili kukabiliana na athari za mvua za hizo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Masoud Amour Masoud, amesisitiza umuhimu wa vijana kuendelea kufanya kazi halali, kushirikiana na viongozi pamoja na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.

Sauti ya Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Masoud Amour Masoud

Nao viongozi wa Gereji zaa Amani, wamewashukuru viongozi hao kwa msaada huo, huku akiomba kuwepo kwa utaratibu maalumu unaowawezesha mafundi kufanya majaribio ya pikipiki baada ya matengenezo bila kukumbana na changamoto ya kukamatwa na polisi.

Sauti vijana gereji.

Aidha amewahimiza vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji na kujiajiri, ili  kujiepusha na vitendo viovu katika jamii.

Sauti za Vijana.