Zenj FM
Zenj FM
20 November 2026, 19:19

Na Ivan Mapunda.
Afisa Uhusiano na Utetezi wa SHIJUWAZA, Hija Shamnte Abdallah, pamoja na Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Nasri Salum Ali, wameeleza umuhimu wa kutoa tahadhari na taarifa sahihi kwa watu wenye ulemavu kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza katika kipindi cha El Niño, wamesisitiza kuwa kundi hilo linahitaji kupewa taarifa kwa njia jumuishi ili kulinda usalama wao.
Wameyasema hayo walipozungumza na Zenj Fm katika kipindi cha Mwangaza wa Habari, huku wakiwataka watu wenye ulemavu kuepuka taarifa za upotoshaji na kufuatilia taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika. Taarifa kamili ungana na Ivan Mapunda