Zenj FM

ZECO yaweka mkakati kuboresha umeme Kaskazini, Kusini Unguja

29 October 2026, 08:48

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linaimarisha upatikanaji wa umeme Kaskazini na Kusini Unguja kupitia mradi wa dola milioni 142, unaohusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na vituo vya kupoza umeme, huku utekelezaji wake ukifikia asilimia 94.

Na Mary Julius.

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limeweka mkakati wa kuboresha upatikanaji wa umeme Kaskazini na Kusini Unguja kupitia ujenzi wa njia mpya za umeme na vituo vya kupoza umeme.

Akizungumza wakati wa ziara ya miradi ya umeme, Meneja Mkuu wa ZECO, Haji Mohamed Haji, amesema mradi huo unalenga kukabiliana na upungufu wa umeme unaochangiwa na ongezeko la mahitaji.

Amesema mradi huo wa dola milioni 142 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unahusisha njia kutoka Welezo hadi Ubago, kisha kuelekea Makunduchi na Matemwe.

Sauti ya Meneja Mkuu wa ZECO, Haji Mohamed Haji.

Aidha meneja ZECO amesema serikali imeamua kuanza zoezi ya kupeleka njia za umeme ardhini ili kutoa nafasi kubwa kwa wananchi kuyatumia ardhi kwa maendeleo na zoezi hilo litaanzia Fumba,

Sauti ya Meneja Mkuu wa ZECO, Haji Mohamed Haji.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi, Maulid Shirazi Hassan, amesema utekelezaji umefikia asilimia 94, huku baadhi ya sehemu zikitarajiwa kukamilika Januari 2027.

Aidha, miradi ya nishati ya jua Bambi na Matemwe inatarajiwa kuongeza megawati 50 kwenye gridi ya taifa, hatua inayolenga kuimarisha huduma ya umeme na kuchochea shughuli za kiuchumi Zanzibar