Zenj FM

RC Hamida awataka watendaji na madiwani kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi

4 November 2026, 15:11

Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Hamida Mussa Khamis akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ATOMIC Dunga Zuze Wilaya ya Kati.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hamida Mussa Khamis, amewataka watendaji na madiwani wa Manispaa ya Kati kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kulinda maslahi ya wananchi

Na Mwandishi wetu.

‎Watendaji wa Baraza la Manispaa Kati wametakiwa kufahamu wajibu wao pindi wanapokua katika majukumu yao ya kazi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Hamida Mussa Khamis ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha madiwani hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa ATOMIC Dunga Zuze Wilaya ya Kati.

Amesema ni jukumu la kila mmoja kusimamia maslahi ya nchi na wananchi pamoja na kusimama katika misingi ya kisheria zinazowaongoza.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Hamida Mussa Khamis

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali Said amesema changamoto kubwa iliyojadiliwa katika kikao hicho ni kutopata magawio kwa wakati ili kuweza kuliongezea baraza hilo mapato.

Sauti ya Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali Said

Nae Msatahiki Meya wa Manispaa Kati Said Hassan Shaaban amewaomba wananchi kutoa mashirikiano kwa baraza hilo ili kuweza kuongeza vyanzo vya mapato kutokana na tozo wanazochangia.

Sauti ya Msatahiki Meya wa Manispaa Kati Said Hassan Shaaban.

‎Adha Baraza la Manispaa Kati katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026/2027 lilipanga kukusanya Jumla ya Shilingi Milioni Miatano na Sabiini na Nane laki tatu Tisini na sita miatano Ishirini na tatu.