Zenj FM

Ushirikiano wa Polisi na wananchi ni muhimu kwa usalama

14 October 2026, 22:21

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Daniel Emanuel Shillah akizungumza na wanachi wa kijiji cha Marumbi Katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Kampeni ya “Ongea na Kamanda” yaanza Kusini Unguja, ikilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi kwa kusikiliza kero zao na kutafuta suluhisho la changamoto za kiusalama. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah, amesema kampeni hiyo itafika shehia zote ili kuimarisha usalama, kupambana na uhalifu na kuweka mazingira salama kwa shughuli za kiuchumi na utalii.

Na Omar Hassan.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Daniel Emanuel Shillah amesema kuanzishwa kwa kampeni ya Ongea Na Kamanda itakuza zaidi mahusiano ya wananchi na Jeshi la Polisi na yatakayowezesha kutatua changamoto za kiusalama.

Akizungumza na wanachi wa kijiji cha Marumbi Katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda Shillah amesema, kufuatia kampeni hiyo Kamanda atakutana na wananchi kwa kupita katika Shehia zote kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Daniel Emanuel Shillah

Nae Mkuu wa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ali Hamadi amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutilia mkazo ushirikiano wa wananchi ili wawe salama na waendelee na shughuli za kiuchumi huku akiwataka wananchi watoe taarifa katika Vituo vya Polisi kwa wakati ikiwemo makosa ya udhalilishaji ili yashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Aidha, amewahimiza Wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kuweka ulinzi katika maeneo ya kitalii ili wananchi waendelee kunufaika na fursa zinazotokana na utalii.

Sauti ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ali Hamadi

Naye Sheha wa Shehia ya Marumbi Juma Hamza Abas amesema kuanzishwa kwa Kampeni ya Ongea na Kamanda italifanya Jeshi la Polisi Kufikika kwa urahisi na wananchi watafaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi.

Sauti ya Sheha wa Shehia ya Marumbi Juma Hamza Abas