Zenj FM
Zenj FM
30 September 2026, 21:53

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuendelea kuwalinda na kuwawezesha wazee ili waishi katika mazingira salama na yenye mahitaji muhimu. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amesema Serikali inafikiria kushusha umri wa uzee kutoka miaka 70 hadi 60.
Na Mwandishi wetu.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuwasimamia wazee ili waishi kwenye mazingira mazuri na kupatiwa mahitaji yote yanayo stahiki.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akil amesema hayo wakati akifungua kongamano la wazee ikiwa ni kuelekea siku ya wazee Duniani.
Amesema Serikali imekuwa ikifatilia kwa karibu changamoto zinazowakabili wazee ili kuhakikisha wazee hao wanaishi katika mazingira salama.
Amesema wazee wamekuwa na mahitaji mengi yanayowakabili hivyo Serikali itawangalia kwa ukaribu ili kuweza kuyatatua
Aidha amefahamisha kuwa Serikali itaangalia namna ya kuzigatia umri wa uzee kutoka miaka 70 ya sasa na kuwa miaka 60.
Nae Katibu wa Jumuiya wastaafu na Wazee Salama ameishukuru Serikali kwa kuwaongezea wazee pecheni pamoja na kuazisha mabaraza ya wazee
Amesema kumekuwa na uzalilishaji mkubwa katika jamii kwa kuwafikiria wazee na vitendo vya ushirikina jambo ambalo halikubaliki.