Zenj FM

Wahitimu wa vyuo watakiwa kuwa mabalozi wa maadili na utii wa sheria

9 July 2026, 15:14

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah akizungumza katika hafla ya kuwaaga wahitimu wa vyuo vikuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, iliyofanyika Kanisa la Waadventista Wasabato Tunguu.

Wahitimu wa vyuo vikuu wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuheshimu sheria za nchi, kuzingatia maadili ya Kanisa na kuishi kwa maadili mema ya jamii. Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah, katika hafla ya kuwaaga wahitimu wa Kanisa la Waadventista Wasabato iliyofanyika Tunguu.

Na Mary Julius.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah, amewataka wahitimu wa vyuo vikuu kuwa mfano bora kwa kuheshimu sheria za nchi, kuzingatia maadili ya Kanisa na kuishi kwa kuzingatia maadili mema ya jamii.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wahitimu wa vyuo vikuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, iliyofanyika Kanisa la Waadventista Wasabato Tunguu, Kamanda Shillah amesema elimu waliyoipata inapaswa kuonekana kupitia mwenendo wao wa kila siku ndani na nje ya Kanisa.

Amesisitiza kuwa wahitimu wanapaswa kuwa mfano unaosomeka na jamii kupitia matendo mema, huku akiwahimiza kujiepusha na makundi ya kihalifu na kutumia mitandao ya kijamii kwa njia yenye tija, ikiwemo kuongeza maarifa, kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya jamii.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah

Kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, Kamanda Shillah amewahimiza wahitimu kuitumia kwa njia yenye tija, ikiwemo kuongeza maarifa, kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya jamii kupitia matumizi sahihi ya teknolojia.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SACP Daniel Emanuel Shillah,

Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tunguu, Mussa Masalu, amesema Kanisa litaendelea kuwalea vijana katika misingi ya amani, kumtanguliza Mungu ili kuwaepuka  na vitendo vinavyokiuka sheria na maadili.

Sauti ya Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tunguu, Mussa Masalu.

Naye mmoja wa wahitimu, Ezekiel Aminiel Abiudi wa Chuo Kikuu cha SUZA, amesema vijana wasomi wanapaswa kuwa chanzo cha maendeleo kwa kutoa elimu sahihi, kusambaza taarifa za kweli na kuwa mfano mwema katika jamii.

Sauti nya Ezekiel Aminiel Abiudi.