Zenj FM

Zenj fm waahidi kutumia mtandao wa Radio Tadio

11 August 2023, 2:43 pm

Waandishi wa Zenj fm wakimsikiliza Mhariri wa Radio tadio Tanzania Hilali Alexander Ruhundwa. Picha na Ahmed

Katika mafunzo hayo waandishi wa Zenj fm wamefundishwa tofauti ya utangazaji wa kwenye Redio na habari za mtandaoni.

Na. Berema Nassor.

Waandishi wa habari wa kituo cha redio cha Zenj FM wameshauriwa kuzitumia fursa zilizopo katika mtandao wa Radio Tadio  ili kuongeza idadi ya wafuatiliaji na wasikilizaji.

Ushauri huo umetolewa na Mhariri wa Radio Tadio Tanzania Hilali Alexander Ruhundwa kwenye mafunzo elekezi kwa waandishi hao ya namna ya kulitumia jukwaa la radio tadio kwa kuchapisha habari zitakazoongeza chachu ya ufuatiliaji kwa wasikilizaji na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Amesema habari zinazovutia wasikilizaji na wafuatiliaji ni zile haswa zinazoigusa jamii hivyo amewahimiza waandishi hao kujikita zaidi kwenye habari za kijamii.

Sauti ya Mhariri wa Radio tadio Tanzania Hilali Alexander Ruhundwa

Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wamesema walikuwa hawatambui fursa za kuongeza wasikilizaji katika kituo chao hivyo sasa wanaandaa mkakati wa kutumia fursa hiyo ya kiteknolojia.

Sauti waandishi wa habari wa Zenj fm