Zenj FM

Wazazi wa kiume watakiwa kutenga muda kwa ajili ya watoto wao

13 August 2023, 4:40 pm

Kundi la wazee na viongozi wa kijamii wakijadiliana jambo juu ya changamoto zinazowakabili watoto na athari zake huko katika ukumbi Makonyo Wawi Chake Chake (picha na Is-haka Rubea. )

Katika kuhakikisha watoto wanakuwa kwenye maadili, wazazi hawana budi kutenga muda wa kuwasikiliza na kuwa karibu nao ili kujenga jamii bora ya badae.

Na. Is-haka Rubea

Wazazi na Walezi wameombwa harakati zao za kutafuta maisha zisiwanyime muda wa kukaa na watoto na familia zao kuwajenga kimaadili’.

Ushauri huo umetolewa na Mratibu Ofisi ya Mrajisi wa Asasi zisizo za kiserikali Pemba Ashrak Hamad Ali alipokuwa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabili watoto uliofanyika huko katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo Wawi Chake Chake.

Amesema changamoto nyingi hasa za ukosefu wa maadili kwa watoto zimekuwa zikichangiwa na mzazi au mlezi wa kiume kuwa mbali na watoto na na kuwaachia jukumu hilo kina mama peke yao.

Sauti ya Mratibu Ofisi ya Mrajisi wa Asasi zisizo za kiserikali Pemba Ashrak Hamad Ali.

Akitoa mada ya changamoto zinazowakabili watoto kwa washiriki wa mkutano huo, Mratibu wa Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar(TAMWA) Fat-hiya Mussa Said ameeleza baadhi ya changamoto zinazowakumba watoto ikiwa ni pamoja na ukosefu wa matunzo kutoka kwa wazazi.

Sauti ya Mratibu wa Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar(TAMWA) Fat-hiya Mussa Said.

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema mporomoko wa maadili katika jamii kunachangiwa kwa kiasi kikikubwa na baadhi ya wazazi na walezi kutosimamia vyema majukumu yao.

Sauti washiriki wa mkutano.