Zenj FM

Zanzibar yaadhimisha siku ya malaria kwa kusambaza vyandarua

25 April 2024, 6:41 pm

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, kisoma hotuba katika maadhimisho ya siku ya malaria duniani yaliyo fanyika Golden Tulip ya uwanja wa ndege mjini Unguja.

Na Mary Julius

Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua juhudi ya kuona ugonjwa wa malaria unaondoka kwa kufanyia kazi kauli mbiu ya mwaka huu usemayo ‘Nipo tayari kushinda malaria Ziro Malaria inaanza na mimi’.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa  wito kwa mikoa ambayo bado ina maambukizi ya malaria kuhakikisha inasimamia vizuri utekelezaji wa mikakati  sahihi ya kumaliza malaria katika maeneo yao ili hatimaye Zanzibar ifikie lengo kuu la kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Akisoma hotuba yake, Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya malaria duniani pamoja na uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua kitaifa sambamba na uzinduzi wa baraza la kumaliza malaria Zanzibar hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip ya uwanja wa ndege mjini Unguja.

Amesema, licha ya kwamba kwa sasa ugonjwa wa Malaria unaendelea kupungua, lakini bado kuna baadhi ya maeneo hususan katika Wilaya za Mjini, Magharibi ‘A’ na ‘B’ maradhi haya yanaendelea kuisumbua jamii.

Rais Dkt. Mwinyi amesema, serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma zote muhimu za afya zinazohitajika kudhibiti malaria zinaendelea kutolewa kwa wananchi wote.

Aidha Rais amewahimiza wananchi kulala ndani ya vyandarua vilivyotiwa dawa na kuendelea kuwahi kufika katika vituo vya afya ili kupatiwa huduma mapema pindi tu wanapojiskia kuwa na dalili za maradhi hayo.

Sauti ya Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui,

Akizungumza katika maadhimisho hayo Meneja wa Program ya Kumaliza Malaria Zanzibar, Dkt. Shija Joseph Shija amesema kwa kipindi cha mwaka 2023   watu laki sita walichunguzwa ugonjwa wa malaria na kati ya hao watu elfu kumi na tisa walipatikana na ugonjwa huo.

Aidha amesema takwimu za hivi karibuni zinathibitisha kwamba vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ni wahanga wa ugonjwa wa malaria visiwani.

Sauti ya Meneja wa program ya kumaliza Malaria Zanzibar, Dkt. Shija Joseph Shija,

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani, Bw. Craig Hart amesema serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) wameungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani na kutangaza kampeni ya usambazaji wa vyandarua.

Sauti ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani, Mr. Craig Hart

Nae Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar, Dk. Salim Slim, ame yapongeza mashirika mbalimbali ambayo yamesaidia katika mapambano dhini ya malaria visiwani Zanzibar huo.

Sauti ya Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar, Dk. Salim Slim

Kaulimbiu ya siku ya malaria ni ‘’NIKO TAYARI KUISHINDA MALARIA, ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI’’

Katika hafla hiyo, Dk. Mwinyi ameteuwa wajumbe wa Baraza la kumaliza malaria Zanzibar akiwemo, Hamza Hassan Juma, Dk. Saada Salum Mkuya, Nassor Ahmed Mazrui, Yussuf Juma Mwenda, Hafsa Hassan Mbamba, Mgeni Hassan Juma, Said Mohamed Said, Yahya Vuai Lada, Asha Juma Khamis.

Wengine ni Aziza Said Ali, Said Salim Bakharesa, Abdusattar Daudi, Ali Amour, Ali Bakari Amani, Shekh Khalid Ali Mfaume, Dk. Martin Stephen Mtolera, Jamal Amour Abdallah (yes Jamal) na Wanu Hafidh Ameir.