Zenj FM

Baraza la Mji Kati laonyesha mfano jinsi ya kutumia tozo

6 September 2023, 3:54 pm

Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati Said Hassan Shaaban akiwa amesima kubadilishana uzoefu wa kazi na wageni kutoka Baraza la Mji Mkoani katika ukumbi wa Baraza la Mji Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Na Mwandishi wetu.

Wananchi wameshauriwa kusimamia maelekezo ya Serikali ikiwemo kudumumisha usafi katika maeneo ya makaazi wanayo ishi.

Mkurugenzi wa Baraza la Mji Mkoani Pemba  Yussuf Kaiza Makame ameyasema hayo katika ziara ya kimafunzo iliyo husisha Madiwani 10, Watendaji 7 kutoka Baraza la Mji Mkoani ziara ambayo imefanyika katika Baraza la Mji Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Aidha Amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza mambo ya maendeleo yanayofanywa na Mabaraza ya Mji, ambapo miongoni mwa hayo ni Usafi, pamoja na kuona namna ambavyo Baraza la Mji Kati lilivyo piga hatua katika suala  la Usafi na kufahamu mbinu ambazo zinasaidia kuleta ufanisi katika suala la ukusanyaji wa mapato katika Baraza hilo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Baraza la Mji Mkoani Pemba  Yussuf Kaiza Makame

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Mji Mkoani Pemba Mohamed Said Ali kwaniaba ya Madiwani wenzake wamelipongeza Baraza la Mji Kati kwa kutumia vyema fedha za tozo kwa kufanya miradi ya ujenzi wa  Soko la Dunga na Soko la Kikungwi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Baraza la Mji Mkoani Pemba Mohamed Said Ali

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati ambae pia ni Diwani wa kuteuliwa  Said Hassan Shaaban kwaniaba ya Baraza la Mji Kati amesema ziara hiyo imejenga mahusiano mazuri Kati yao na kubadilishana uzoefu wa kazi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati Said Hassan Shaaban

Maeneo yaliyo tembelewa na ujumbe huo kutoka Baraza la Mji Mkoani ni Soko la wananchi Dunga, Karakana iliyopo Hanyegwa Mchana na   Soko la Mazao ya Baharini lililopo Kikungwi.