Zenj FM

Polisi Kusini Unguja kuimarisha ulinzi sikukuu ya Eid el Fitr

9 April 2024, 7:40 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Daniel Emanuel Shilla.

Na Mary Julius.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja SACP Daniel Emanuel Shilla amesema jeshi la polisi limejipanga katika kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika kipindi chote cha sikukuu ya Eid el Fitr.

Kamanda ameyasema hayo wakati akizungumza na Zenj Fm makao makuu ya polisi mkoa wa
Kusini Unguja. Amesema katika kusheherekea sikukuu hiyo jeshi la polisi  mkoani humo limejipanga kuimarisha ulinzi katika sehemu zote za kufurahishia watoto  pamoja na maeneo ya fukwe za bahari.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto na vitendo vya udhalilishaji kwa kuhakikisha watoto wanaongozana na watu wazima katika viwanja vya kufurahishia watoto.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika hatua nyingine kamanda Daniel amewataka madereva kuwa makini katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kuendesha vyombo vya moto kwa kufuata sheria za usalama barabarani.  

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja.