Zenj FM

Asma Mwinyi arejesha matumaini kwa wanafunzi wa kike Zanzibar

7 September 2023, 5:07 pm

Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Mwinyi akiwa na wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kwarara mara baada ya kuwagawia taulo za kike.

Na Mary Julius

Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Mwinyi amesema taasisi hiyo inaandaa mkakati wa kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa kike kwa kuwajengea vyoo maskulini ili kuondoa changamoto zote zinazowakumba  wanapo kuwa katika hedhi.

Asma ameyasema hayo mara baada ya kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa skulii ya sekondari ya kwarara ikiwa ni muendelezo wa kugawa taulo hizo kwa wanafunzi wa skuli za jimbo la dimani akishirikiana na umoja wa wanawake wa jimbo hilo  amesema lengo ni kuweka mazingira rafiki yatakayo wezesha mwanafunzi kike kusoma vizuri.

Aidha Asma amewaahidi wanafunzi wa skuli ya sekondar ya kwarara wanaotarajia kufanya mitihani ya kidato cha nn iwapo watafauli kwa daraja la mwanza atawapatia mabunda matano ya taulo za kike  kwa kila mmoja.

Sauti ya Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Mwinyi

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Skuli ya sekondari ya kwarara Khadija Sharif Omary ,ameipongeza taassisi hiyo kwa kuweza kutoa taulo hizo na amewaomba zoezi  hilo liwe  la mara kwa mara kwani uhitaji ni mkubwa.

Sauti ya Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Skuli ya sekondari ya kwarara Khadija Sharif Omary

Kwa upande wake  diwani wa viti maalum Veronika Pang`las Mtindira amesema UWT dimani kwa kushirikiana na asma mwinyi faoundation imejipanga kutoa taulo za kike kwa skuli zote zilizopo katika wilaya ya dimani kichama lengo likiwa ni kuwawezesha watoto wa kike kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika masomo yao.

Sauti ya Diwani wa viti maalum Veronika Pang`las Mtindira

Nao wanafunzi wa skulii ya kwarara wameishukuru asma mwinyi faundatuon kwa kuweza kuwapata taulo hizo zitakazo wasaidia kujistili.

Sauti ya wanafunzi wa skuli ya sekondar ya Kwarara

Zaidi ya wanafunzi 600 wa skuli ya kwarara secondary wamepatiwa taulo hizo za kike.