Zenj FM

Jamii yahimizwa kusaidia makundi maalum

13 March 2024, 5:04 pm

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa Mkoa wa Kusini Unguja Makama Ramadhan Mbanja (wa pili kushoto) akikabidhi vyakula kwa mwalimu mkuu na wanafunzi wa skuli ya Hasnuu Makame.

Na Mary Julius.

Jamii nchini  imehimizwa  kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kukithirisha kufanya ibada kwa kusaidia mahitaji  katika makundi mbalimbali ya  kijamii ikiwemo elimu ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mapolo ya vyakula vyenye thamani ya zaidi ya shiling milioni nne  kwa wanafunzi wa skuli ya Hasnuu Makame iliyopo Kibuteni, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa Mkoa wa Kusini Unguja Makama Ramadhan Mbanja amesema  ameona umuhimu wa kutoa msaada  huo katika skuli hiyo kutokana na kuwa ya  bweni na ina wanafunzi wa makundi mbalimbali ikiwemo yatima,  walemavu na wenye mazingira magumu hivyo  utolewaji wa  msaada huo utawapelekea wanafunzi hao kusoma  masomo yao kwa uhakika.

Aidha mjumbe huyo amesema  hatasita kutoa misaada kama hiyo katika skuli zingine na kwa jamii ili  kuona kwamba wanafunzi wanaondokana na uhaba wa futari hasa katika kipindi hiki.

Sauti ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Kusini Unguja Makama Ramadhan Mbanja

Mwalim Mkuu wa skuli hiyo Bakari Mohd Ali amezipongeza juhudi za mjumbe huyo kwa kujitoa kwake  na kuona umuhimu kwa kusaidi skuli hiyo na kuahidi vyakula hivyo watavitumia kama ilivyokusudiwa.

Sauti ya Mwalim Mkuu wa skuli hiyo Bakari Mohd Ali

Nao mwanafunzi wameshukuru Kwa msaada huo na kuomba taasisi na watu wenye uwezo  kuiga mfano kama huo  kwa lengo la kupata radhi za Allah pamoja na kukuza  ustawi wa wanafunzi na elimu kwa ujumla.

Sauti ya wanafunzi

Vyakula vilivyokabidhiwa ni pamoja na  maharage gunia 5, unga wa ngano  Pakti 7, sukari 4, tende, mchele, na mafuta ya kupikia box 4