Zenj FM
Zenj FM
2 May 2026, 9:28 pm

ZFDA imeteketeza tani 4.8 za maziwa ya watoto aina ya SMA kwa tuhuma za kubainika kuchafuliwa na bakteria hatari. Uchafuzi huo unaweza kusababisha madhara kama kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo na kuharisha.
Na Mary Julius/
Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZFDA) umeteketeza tani 4.8 za maziwa ya watoto aina ya SMA baada ya kubainika kuchafuliwa na sumu ya cereulide kutoka bakteria ya Bacillus cereus.
Afisa Uhusiano ZFDA, Fatuma Makame Juma, amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia taarifa kutoka kampuni ya Nestlé na ukaguzi uliobaini bidhaa hiyo si salama, ikiwa na madhara kama kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo na kuharisha.
ZFDA imewahakikishia wananchi kuwa maziwa yaliyopo sokoni (namba 2 na 3) ni salama, na kuwataka wafanyabiashara kushirikiana kutoa taarifa za bidhaa hatarishi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Bopar Enterprises, Abdul Hussen Mohamed, amesema kwa kushirikiana na ZFDA wamefanikiwa kutoa maziwa hayo na maziwa yaliyobaki madukani yanafaa kwa matumizi ya binaadamu na kuahidi kuendeleza mashirikiano hayo ili kuepuka athari za bidhaa zilizokwisha muda wake.