Zenj FM

CUF yasisitiza maridhiano ya kisiasa, yamtaka Katambi kuitisha kikao cha vyama

5 July 2026, 08:02

Mkurugenzi wa Matukio na Siasa wa chama hicho, Ali Makame Issa, akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CUF, Mtendeni, Zanzibar.

Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia upya uamuzi wa kuzuia mikutano ya kisiasa, kikisisitiza kuwa mazungumzo kati ya vyama ndiyo njia bora ya kuimarisha demokrasia, maridhiano na utulivu wa kisiasa nchini. Aidha, chama hicho kimeitaka Serikali kuhakikisha ajira zinatolewa kwa uwazi na haki, huku kikitangaza hatua za kisheria dhidi ya watakaobainika kuhodhi au kuiba mali za chama.

Na Mary Julius.

Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kupitia upya uamuzi wa kuzuia mikutano ya kisiasa na kuitisha kikao cha viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuimarisha demokrasia, maridhiano na mazingira bora ya kisiasa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CUF, Mtendeni, Zanzibar, Mkurugenzi wa Matukio na Siasa wa chama hicho, Ali Makame Issa, amesema mazungumzo ndiyo njia bora ya kutatua tofauti za kisiasa kuliko migogoro ya mahakamani, huku akisisitiza kuwa hatua za kiusalama zisinyime vyama haki ya kufanya shughuli zao za kisiasa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Matukio na Siasa wa chama hicho, Ali Makame Issa.

Ali amesema uongozi mpya wa CUF umeanza kukijenga upya chama kwa kuimarisha mshikamano na utatuzi wa migogoro ya ndani, huku ukijiandaa kufanya ziara katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kusikiliza kero za wananchi na kuimarisha chama.

Sauti ya Mkurugenzi wa Matukio na Siasa wa chama hicho, Ali Makame Issa.

Kuhusu ajira, amepongeza juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali, lakini ameitaka Serikali kuhakikisha nafasi za kazi zinatangazwa na kutolewa kwa uwazi, usawa na haki.

Aidha  amewataka wanachama waliohama CUF kurejesha mali za chama walizonazo, akionya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhodhi au kuiba mali za chama.

Sauyi ya Mkurugenzi wa Matukio na Siasa wa chama hicho, Ali Makame Issa.