Zenj FM

Uzalishaji taka waongezeka Zanzibar kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

27 March 2024, 6:43 pm

Eneo la kuwekea taka shehia ya Mikunguni. Picha na Rahma Hassan.

Na Rahma Hassan.

 Kuelekea katika kipindi cha mvua za masika wakaazii wa shehia ya mikunguni wameliomba Baraza la Manispaa Zanzibar kulitafutia ufumbuzi suala la taka  zilizozagaa katika jaa la shehia yao.

Wakizungumza  na zenji FM Wananchi hao  Wamesema   karibu wiki tatu sasa wazoaji wa taka katika shehia hiyo hawajafika kuzichukua hali ambayo inahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo

Aidha wamesema katika eneo hilo la jaa kulikuwepo kikapu cha kuwekea taka lakini baraza hilo limekiondoa na kusababisha kuzagaa ovyo kwa taka.

Sauti ya wakaazi wa shehia ya mikunguni.

    Nae  sheha  wa shehia ya mikunguni Makame KHatib Amesema uwezo wa manispaa wa kukusanya taka umepungua hali ambayo imepelekea kuzagaa kwa taka hizo.

Sauti ya sheha wa shehia ya Mikunguni Makame Khatibu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Ali Khamisi Mohd amekiri kuwepo kwa tatizo hilo  ambalo limesababishwa na uchakavu wa vikapu vya kuwekea taka katika majaa mbalimbali Zanzibar.

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Ali Khamisi Mohd