Zenj FM

Mishahara mipya Zanzibar, walimu na madaktari kunufaika

20 October 2026, 23:32

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Dkt. Harroun Ali Suleiman.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaweka wazi kuwa mishahara mipya itawanufaisha walimu wa maeneo tengefu, madaktari na watumishi wengine wa umma. Waziri Dkt. Haroun Ali Suleiman ameelezea makundi yatakayonufaika na mabadiliko hayo pamoja na wito kwa watumishi kutekeleza majukumu yao kwa bidii na uaminifu.

Na Is-haka Mohammed. Pemba

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema mishahara mipya kwa watumishi wa umma Zanzibar iliyotangazwa kuongezwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na kuwanuafaisha watendaji katika taasisi zote za umma nchini, pia imewazingatia wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira magumu na maeneo tengefu.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari huko katika Ukumbi wa ZRA Gombani Chake Chake, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Dkt. Harroun Ali Suleiman  ametaja miongoni mwa watumishi hao ni pamoja na walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu na maeneo tengefu, wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum, maofisa wa elimu wa Wilaya na Mikoa, madaktari na madaktari dhamana wa wilaya.

Amesema mabadiliko hao yameangalia katika mihimili yote mitatu ya serikali Mahakama na Bazara la Wawakilishi na serikali na wote watafaidika na mabadiliko hayo ya mishahara wakiwemo watendaji wa watumishi katika ofisi za viongozi wakuu na wanaofanya kazi za faragha.

Sauti ya Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Dkt. Harroun Ali Suleiman.

Aidha Waziri Haroun amewahimiza watumishi wa umma katika taasisi mbali mbali kutekeleza  wajibu wao wa kiutendaji kwa bidii na uaminifu na serikali itaendelea kuwazingatia maslahi yao kwa hali na mali.

Sauti ya Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Dkt. Harroun Ali Suleiman.