Zenj FM

Matumizi holela ya dawa yatajwa kuchochea usugu wa vimelea

19 November 2026, 14:27

Msimamizi wa Kitengo cha Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Nadra Yusuf,Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Wiki ya Uhamasishaji kuhusu Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, katika ukumbi wa Wizara ya Afya Zanzibar.

Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kushirikiana na Serikali kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki ili kudhibiti ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa. Wananchi pia wametakiwa kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa wataalamu wa afya na kuhakikisha wanakamilisha dozi wanazoelekezwa.

Na N

Msimamizi wa Kitengo cha Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Nadra Yusuf, amewaomba waandishi wa habari kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Wiki ya Uhamasishaji kuhusu Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, inayoadhimishwa Novemba 18 hadi 24, amesema waandishi wa habari wanapaswa kutumia taaluma yao katika kuwaelewesha wananchi ili  waepuke  kutumia antibiotic bila maelekezo ya daktari na kufuata maelekezo ya matumizi ya dawa.

Amesema matumizi holela ya dawa hizo katika afya, kilimo na ufugaji yanachangia kuongezeka kwa usugu wa vimelea, huku takwimu za kimataifa zikionyesha tatizo hilo lilihusishwa moja kwa moja na vifo milioni 1.14 duniani mwaka 2021 na kuchangia vifo milioni tano.

Sauti ya Nadra Yusuf.

Katika kukabiliana na tatizo hilo Nandra amesema Zanzibar imeandaa mpango kazi wa taifa wa kukabiliana na tatizo hilo kwa kushirikisha sekta mbalimbali ili kuimarisha udhibiti wa dawa.

Aidha Nadra ameewataka Wauzaji wa dawa kuzingatia taratibu na maelekezo ya wataalamu wa afya katika utoaji wa dawa za antibiotic ili kudhibiti matumizi holela yanayochangia usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Sauti ya Nadra Yusuf,

Kwa upande wake, Raifa Simai Ali kutoka kitengo cha usugu wa dawa amesema kutokamilisha dozi na kutumia dawa bila ushauri wa wataalamu kunaweza kuongeza usugu wa vimelea, hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

Sauti ya Raifa Simai Ali.