Zenj FM

Polisi Zanzibar kutumia kamera kupambana na makosa barabarani

13 September 2026, 22:29

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Haji Mkali Haji Akifungua Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa kamera katika kufuatilia makosa ya Usalama barabarani.

Jeshi la Polisi Zanzibar limeanza kutumia teknolojia ya kamera katika kufuatilia makosa ya usalama barabarani, hatua inayolenga kupunguza ajali, kuimarisha utii wa sheria na kuokoa maisha.

Na Omar Hassan.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Haji Mkali Haji amesema matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa Usalama barabarani ni hatua muhimu katika kulifanya Jeshi la Polisi liendane na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya jamii ya sasa.

Akifungua Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa kamera katika kufuatilia makosa ya Usalama barabarani, Kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, yaliyowahusisha Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar, leo Septemba 13, 2026 huko chuo cha Polisi Zanzibar amesema Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa mfumo huo unatumiwa kwa ufanisi na kwa weledi.

Aidha ameeliza kuwa Mfumo wa kamera utasaidia kjupunguza makossa ya usalama barabarani, kupunguza ajali, kuimarisha utii wa sheria na kuokoa maisha.

Sauti ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Haji Mkali Haji

Nae Mkurugenzi wa Usalama Mamlaka ya Usafiri na usalama barabarani Zanzibar Fadhil Juma Ali kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo amesema Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar itaendelea kushiriliana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti makosa ya usalama barabarani

Sauti ya Mkurugenzi wa Usalama Mamlaka ya Usafiri na usalama barabarani Zanzibar Fadhil Juma Ali