Zenj FM

Utalii Pemba wafungua milango ya fursa kwa vijana, wanawake

28 September 2026, 13:26

 Mkuu wa Wilaya ya  Chae Chake Zuhura Mgeni Othman akizungumza na wadau wa utalii alipokuwa akifungua Kongamano la Siku ya Utalii Duniani.

Kuongezeka kwa uelewa kuhusu utalii na ushirikiano wa wadau kunatajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayosaidia kukuza sekta hiyo Pemba. Serikali na wadau wanaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha fursa za utalii zinawanufaisha zaidi wananchi wa ndani.

Na Is-haka Mohammed Pemba.

Mashirikiano Mazuri kati ya Wadau wa Utalii na Serikali kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya watalii wanaofika kisiwani Pemba.

Akifungua Kongamano la Siku moja la Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani lililowashirikisha wadau mbali mbali wa utalii kisiwani Pemba huko Tibirinzi Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Zuhura Mgeni Othman amesema mashirikiano hayo yamesaidia sana kukuza sekta hiyo kisiwani Pemba.

Amesema mwanzoni suala la Utalii kisiwani Pemba lilikabiliwa na changamoto kubwa zilizotokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya utalii.

 Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya  Chae Chake Zuhura Mgeni Othman.

Kwa upande wake Mratibu wa Kamisheni ya Utalii Pemba Moh`d Walid Fikirini amesema wameandaa Programu maalum ya kutoa elimu kwa wadau wa utalii wajasiriamali na makundi mengine katika hatua ya kukuza uelewa zaidi juu ya utalii Pemba.

Sauiti ya Mratibu wa Kamisheni ya Utalii Pemba Moh`d Walid Fikirini.

Mkurugenzi wa Safari Gats Away Limited Biubwa Omar Khamis amesema ni vyema vijana, wanawake, watu wenye ulemavu na wananchi wa vijijini kuchangamkia fursa zitokanazo na utalii mapema ili fursa hizo ziwanufaishe na wasitoke watu mbali kuja kupata fursa hizo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Safari Gats Away Limited Biubwa Omar Khamis.