Zenj FM
Zenj FM
12 November 2026, 16:24

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hamida Mussa Khamis, amezindua wito wa kampeni ya usalama barabarani kwa kuwaelimisha waendesha bodaboda kuzingatia sheria, kupunguza mwendo na kuvaa kofia ngumu. Kampeni hiyo inalenga kupunguza ajali na kuokoa maisha ya wananchi kwa kaulimbiu: “Punguza Mwendo, Vaa Kofia Ngumu, Fika Salama.”
Na Omar Hassan
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Hamida Mussa Khamis amewataka waendesha Pikipiki maarufu kama bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za barabarani katika Mkoa huo.
Akizungumza na waendesha bodaboda na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Tamasha la Kampeni ya kupunguza ajali za barabarani huko Tunguu, Wilaya ya KATI Mkoa wa Kusini Unguja amewataka kuchukuwa hatua za kupunguza ajali ikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutopakia zaidi ya abiria mmOja na kuacha kwenda mwendo wa kasi.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Emanuel Shillah amesema Jeshi la Polisi limekuwa likichukua hatua za kukabiliana na ajali za barabarani ikiwemo kutoa elimu ya utii wa sheria bila ya shuruti sambamba na kuwakamata madereva wasiotii Sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Usafiri Barabarani Kamishna Msaidizi wa Polisi Mstaafu Mkadam Khamis Mkadam amesema lazima Waendesha bodaboda kupata mafunzo ya udereva ili kuepuka ajali ambazo zinaongeza umasikini wa mtu mmoja mmoja, Jamii naTaifa.
Akisoma risala ya Waendesha bodaboda Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Kati Ali Rajab Jaffar wameomba kupunguzwa gharama za leseni kutokana na bodaboda wengi wanashindwa kuwa na leseni kutokana na gharama kubwa.
Kauli mbiu ya tamasha hilo ni Bodaboda Punguza Mwendo, Vaa Helmet, Fika Salama.