Baraka FM

Wawili wafariki Mgodini Chunya Mbeya

21 January 2025, 19:25

Kwenye maisha changamoto zinamfanya mtu wajibiki kuhakikisha jamii yake inakuwa vizuri,na hii huwafanya watu wengi kutafuta maisha kwa kufanya kazi inayoonekana mbele yake.

Na mwandishi wetu

Watu wawili waliotajwa kwa majina ya Daniel Mwendesha (26) na Sam Sagali (25) wamepoteza maisha kutokana na ajali ya kufukiwa na kifusi kwenye mgodi wa madini ya dhahabu wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa madini hayo katika Kijiji cha Itumbi, Wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Mbeya, Malumbo Ngata, amesema tukio hilo lilitokea Januari 12, mwaka huu wakati akizungumza na moja ya chombo cha habari hapa nchini leo Januari 21, 2025.

Kamanda Ngata amesema kuwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi, askari wa kikosi cha uokozi walifika eneo la tukio na kufukua kifusi hicho ambapo walikuta miili ya watu wawili wakiwa wamepoteza maisha kwa kukosa hewa.