Baraka FM

Wagonjwa wa kipindupindu Mbeya jiji wafikia 46

18 December 2024, 12:21

Hawa ni wageni wakiwa ndani ya studio za Baraka FM kutoa elimu ya makabiliano ya ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu (picha na Hobokela Lwinga)

Uwepo wa mvua umesababisha uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya.

Na Hobokela Lwinga

Halmashauri ya Jiji la Mbeya limethibisha uwepo wa wagojwa 46 wa kipindupindu kuanzia december 06,2024.

Taarifa ya uwepo wa wagojwa hao imetolewa na afisa afya Kulwa Kihinga wakati akitoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa huo katika kipindi cha nuru ya asubuhi kinachorushwa baraka fm redio kwa ushirikiano na taasisi ya empowercare foundation.

Kihinga amesema serikali imeendelea na mapambano ya kukabiliana na ugonjwa kwa kutoa elimu katika maeneo ambayo ni hatari na yanaweza kusababisha ongezeko la mlipuko ikiwemo sokoni na kwenye mikusanyiko ya watu.

Afisa afya Kulwa Kihinga (katikati)picha na na Hobokela Lwinga
Sauti ya Afisa afya Kulwa Kihinga

Kwa upande wake afisa afya Uswege Msomba amesema ugonjwa huo unatokana na kula kinyesi cha binadamu huku akitaja dalili zake kuwa ni mtu kutapika na kuharisha maji maji yenye rangi ya mchele.

Afisa afya Uswege Msomba(kulia)picha na Hobokela Lwinga)
Sauti yaAfisa afya Uswege Msomba

Hata hivyo afisa afya Roswita Lusambo amesema katika jiji la Mbeya kata 18 wamepatikana wagonjwa kipindupindu,ameongeza kuwa pia vipo vyuo ambavyovimebainika kuwa wagonjwa kikiwemo chuo kikuu cha kikatoliki Mbeya CUoM

Afisa afya Roswita Lusambo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya afisa afya Roswita Lusambo

Nao baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ili jamii inedelee kuchukua tahadhali ya kukabiliana na ugonjwa huo.