Baraka FM

DC Haniu afanya ziara Shule ya amali

9 January 2025, 18:19

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh Jaffar Haniu akiwa na viongozi mbalimbli katika Shule ya Amali

kutokana na mabadiliko mbalimbli ya mitaala ya Elimu serikali inaendelea na ujenzi wa Shule zitakazo kidhi mitaala hiyo.

Na mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu leo tarehe 9.1.2025 amefanya ziara na kukagua hatua ya ujenzi wa shule ya Amali (Ufundi) iliyopo katika kata ya Kisondela.

Mwonekano wa majengo ya Shule ya Amali mpaka sasa

Mhe Haniu pamoja na mambo mengine ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kuwa hii itasaidia ukuaji wa maarifa na ujuzi kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe mara ujenzi utakapokamilika.

Katika hatua nyingine Mhe Haniu ameagiza mafundi wanaotekeleza mradi huu kufanya kazi usiku na mchana ili kusaidia ukamilishaji kwa wakati.

Mheshimiwa Jaffar Haniu akitoka maagizo kwa mafundi wanao tekeleza ujenzi wa majengo hayo

Kwa upande wa wanannchi wameshukuru serikali kwa kujenga shule hiyo katika kata yao kwani imeongeza ajira katika hatua ya ujenzi pia itachavusha uchumi kwani wanafunzi pamoja na watumishi wa shule hii watanufaika na bidhaa za kilimo zinazozalishwa katika eneo hili maarufu kwa kilimo cha ndizi, parachichi, machungwa, mahindi na karanga.

Jumla ya Shilingi Million 583 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule hii ambayo Baraza la Madiwani tayari limetoa azimio la kusajiliwa kwa jina la Renatus Mchau Mchau mara ujenzi wake utakapokamilika.