Baraka FM

Vijana KMT-JKM wafanya mkutano mkuu Songwe

12 October 2024, 09:33

kumalizika kwa Mkutano mkuu wa Jimbo kwa kanisa la Moravian Tanzania kunatoa fursa kwa vijana hao kuanza maandalizi ya mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania (KMT) ambao utafanyika jijini Dodoma.

Na Hobokela Lwinga

Vijana kati wa kanisa la Moravian tanzania jimbo la kusini magharibi wameanza mkutano wao mkuu wa jimbo unaofanyika katika ushirika wa mkwajuni halmashauri ya Songwe.

Katika mkutano huo vijana hao wanatarajia kujifunza masomo mbalimbali katika nyanja ya uchumi, ndoa sambamba na kubadilisha vipawa vya uimbaji na usomaji wa Bilblia.

Aidha mkutano huo umejumuisha vijana kutoka wilaya nne za kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi ambazo ni Mbeya,Chunya, Mbalizi na Mbarali.

Ikumbukwe kuwa mkutano huo umeanza alhamisi october 10, na utamalizika october 13,2024.