Baraka FM

Chanzo Cha ajali mfululizo Mbeya chatajwa

7 October 2024, 22:57

kutokana na kushamili kwa ajali nyingi nchi zinazohusisha vyombo Vya Moto chanzo hatujawa

Na Ezekiel Kamanga

Uzembe wa madereva, ukosefu wa alama za barabarani,ubovu wa mabasi na miundombinu ya barabara Mkoani Mbeya umesababisha vifo vya watu thelathini na tatu na majeruhi themanini na sita katika ajali tatu tofauti katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

Hayo yamebainishwa na Kamishina wa Polisi oparesheni na mafunzo Awadh Haji katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya huku akieleza lengo la ziara yake kuwa ni pamoja na kukagua maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi na masuala ya usalama barabarani.

Kwenye masuala ya uchaguzi amesema maandalizi yote yapo vizuri ikiwa ni pamoja na mazoezi ya utayari kwa askari.

Awadh amesema ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva pamoja na kutokuwepo kwa alama za usalama barabarani pia miundombinu mibovu ya barabara.

Katika hatua nyingine Kamishina wa Polisi oparesheni na mafunzo Awadh Haji amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa hali ya usalama ni shwari na Jeshi la Polisi limejipanga ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema watayafanyia kazi maelekezo yote.

Madereva na watumiaji wa barabara watazingatia maelekezo kutasaidia kupunguza ajali nchini sanjari na kudumisha amani katika uchaguzi.