Baraka FM

Mchungaji Andrea Simbeye azikwa nyumbani kwake Iwambi Mbeya

17 September 2024, 22:11

Kila nafsi itaonja mauti vitabu vitakatifu vimeandika , na hii inadhihilisha kuwa duniani tunasafiri hivyo tunapaswa kuendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu.

Na Hobokela Lwinga

Mchungaji mstaafu marehemu Andrea Simbeye aliyefariki dunia September 14,2024 amezikwa leo Septemba 17,2024 nyumbani kwake Iwambi Jijini Mbeya.

Ibada ya mazishi imehudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi na ibada hiyo imefanyika katika ushirika wa Iwambi.

Akisoma wasifu wa marehemu, Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israel Mwakilasa amesema marehemu amefariki kwa magonjwa ya athima,shinikizo la damu, kisukari na kiharusi.

Aidha Katibu Mkuu Mwakilasa amesema alikuwa mkristo rasmi na alibatizwa mwaka 1963 katika ushirika wa kapele uliopo Momba mkoani Songwe.

Mchungaji mstaafu marehemu Andrea Simbeye

Katibu Mkuu huyo amesema mchungaji mstaafu marehemu Andrea Simbeye amelitumikia kanisa katika nafasi mbalimbali sambamba na kuwa mchungaji katika shirika.

Ibada hiyo licha ya kuhudhuriwa na Watu mbalimbali pia mhashamu baba Askofu Robert Yondam Pangani amekuwa sehemu ya waombolezaji.