Baraka FM

Moravian JKM yathibitisha kifo cha Mch. Andrea Simbeye

15 September 2024, 16:39

Mchungaji mstaafu marehemu Andrea Simbeye

Duniani hakuna mwenye makazi ya kudumu hivyo inatupasa kujiandaa ili kuwa na mwisho mwema.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi linatangaza kifo Cha mchungaji mstaafu marehemu Andrea Simbeye kilichotokea tarehe September 14,2024.

Taarifa iliyotolewa na makamu mwenyekiti wa kanisani la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende anaeleza kuwa marehemu amefariki dunia Wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya.

Makamu mwenyekiti wa kanisani la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende

Mchungaji Mwahalende amesema ibada ya kumuaga marehemu mch.Simbeye itafanyika September 17,2024 katika ushirika wa Iwambi kuanzia saa nne asubuhi na kisha kuzikwa nyumbani kwake Iwambi.

Katika taarifa hiyo makamu wa mwenyekiti amewataka Watu wote kuendelea kuiombea familia ili Mungu aendelee kuwa faraja kwao.