Wakristo watakiwa kuwa na upendo
24 June 2024, 17:53
Umoja wa wakristo wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi wameombwa kuwa na upendo baina yao katika kuitenda kazi ya Mungu.
Na Lukia Chasanika
Katibu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzani Jimbo la Kusini Magharibi Israel Mwakilasa amewataka wakristo kuwa na upendo wa kweli miongoni mwao ili kudumisha mshikamano ndani ya kanisa.
Mwakilasa amesema hayo wakati akihubiri katika mkutano wa vijana kati dinari ya songwe uliofanyika kanisa la Moravian ushirika wa Nanyala mkoani Songwe.
Mwakilasa amesema kanisa linatakiwa kuwa na umoja kama vitabu vitakatifu vinavyoeleza juu ya kumpenda Mungu pamoja na jirani yako.
Kwa upande wake mlezi wa idara ya vijana kati dinari ya songwe Mch Daniel Sichone amesema katika idara hiyo wanafundisha masomo mbalimbali ikiwemo ndoa,uchumi na uchumba kwa vijana ambao hawajaoa na kuolewa namna gani wanaweza kumpata mchumba na hatimae kuwa na ndoa takatatifu.
Aidha msimamizi wa uimbaji Joseph Masasa amesema vijana wanatakiwa kujifunza namna ya kutumia manoti ya mziki ili kwenda sawa na upigaji wa vyombo vya mziki kama kinanda.
Hata hivyo mwenyekiti wa idara ya vijana kati dinari ya Songwe Andrew Mwakalinga amesema kichwa cha mkutano kilikuwa ni kutoipenda dunia na mamboa yake yote hivyo amewashauri vijana kuipenda idara hiyo ili waweze kujifunza neno la Mungu.
Mmoja wa vijana walifanya mtihani wa bibilia na kushika nafasi ya kwanza Anna Kaminyoge kutoka ushirika wa songwe amesema utofauti uliopo katika ya kusoma biblia na uimbaji ambapo ameeleza kuwa biblia inamuimarisha mtu binafsi lakini uimbaji ni kuhubiri kwa watu wengine.