Baraka FM

Wanawake jitokezeni kupata mafunzo ya kujenga ndoa zenu

3 May 2024, 09:48

Mchungaji Prisca Mwasansu akifundisha semina ya wanawake Mbalizi Mbeya(picha na Iman Anyigulile)

Kutokana na utandawazi kuendelea kukua katika ulimwengu huu wanawake wametakiwa kujitokeza katika semina mbalimbali kujifunza namna bora ya kuishi kwenye ndoa zao.

Na Iman Anyigulile

Wanawake mkoani Mbeya wametakiwa kujifunza mara kwa mara mafundisho ya ndoa ili kuweza kuimarisha ndoa zao na kujari familia zao.
Hayo yameleezwa na mchungaji Prisca Mwasansu wakati alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la wanawake lililofanyika katika kanisa la RGC Victori mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.

Sauti ya mchungaji Prisca Mwasansu

Mch Mwasansu amesema kuwa mwanamke anatakiwa kuwa na uwezo wa kufikiri , kuamua na kutenda lengo ni kupata watu walio sahihi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii.

Baadhi ya wanawake walio shiriki semina hiyo(picha na Iman Anyigulile)
Sauti ya mchungaji Prisca Mwasansu

kwa upande wao wanawake walioweza kuhudhuria kongamano hilo wamesema kuwa kupitia kongamano hilo wamejifunza namna bora ya kuwa na uvumilivu katika ndoa na mwanamke kuwa jasiri na kiungo katika familia.

Sauti za baadhi ya wanawake walio hudhuria kongamano