Moravian chini ya Mission 21 yafanya tathmini ya miradi
11 May 2024, 10:52
Wafadhili wa Mission 21 katika kanisa la Moravian Tanzania wamekutana na jimbo la kusini magharibi na jimbo la kusini na wasimamizi wa miradi mbalimbali ili kufanya tathimini ya miradi iliyo pita kwa mwaka 2022-2024 na kupokea maoni ya miradi ujao 2025-2028.
Na Ezra Mwilwa
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi na Jimbo la kusini wamefanya warsha na wafadhiri wa mradi misheni 21 kujua changamoto zinazokwamisha kukua kwa uchumi vijijini.
Msimamizi wa mradi huo Adrienne Sweetman amesema lengo la kufanya washa hiyo ni kufanya tathimini ya miradi iliyotekelezwa mwaka 2022-2024 na kupokea maoni ya mradi ujao 2025-2028.
Baadhi ya washiriki katika washa hiyo wanawapongeza wafadhiri hao kwa kuwakutanisha ili kujua changamoto wanazopitia.
Aidha wameongeza kuwa wanaamini baada ya kuchukuliwa kwa maoni ya msimu ujao 2025-2028 na kufanya maboresho yatakayosaidia kutekeleza kwa wakati mwafaka kazi zao.
Kaulimbiu katika warsha hiyoni “Uwezeshaji wa kiuchumi katika maeneo ya vijijini”