Askofu Panja: Tendeni mema ili mkumbukwe
21 November 2023, 19:34
Na Hobokela Lwinga
Askofu mteule wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani amewataka wananchi nchini kutunza amani iliyopo kuanzia kwenye maeneo yao wanayoishi badala ya kuwa wavunjifu wa amani.
Hayo ameyasema katika ibada ya msiba wa kumuuga marehemu mch.sifael mwashibada katika ushirika wa meta jijini mbeya .
Mch.Pangani amesema kila mwananchi anapaswa kuepuka makundi maovu yenye viashiria vya uvunjifu wa amani badala yake wanapaswa kuwa wanyenyekevu na kuomba toba kwa Mungu.
Akihubiri katika ibada ya mazishi katika ushirika wa Karasha Mbozi Songwe askofu Keneni Panja wa kanisa la Moravian jimbo la kusini amesema kila mtu anapaswa kutenda ili aweze kukumbukwa duniani na mbinguni.
Hata hivyo askofu wa makanisa ya Brotherhood Tanzania askofu Rabi Mwakanani aliyefika katika ibada ushrikani Meta kuungana na waombolezaji kumuuga mch.Mwashibanda amesema mch.Mwashibanda atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwemo unyenyekevu na uchaji kwa Mungu.
Sambamba na hayo akisoma wasifu wa marehemu ,katibu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi ndugu Israel Mwakilasa amesema enzi za uhai wa mch.Mwashibanda amehudumu katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirikani,idara pamoja na taasisi za kanisa.
Aidha viongozi wa mtaa wa Kajigili unapopatikana ushirika wa Meta wamesema kwao wamepata pengo kubwa kwani mchungaji huyo alikuwa mshauri mzuri katika kuchochea maendeleo kwenye mtaa huo.
Mch.Sifael Mwashibanda amezikwa katika eneo la karasha Mlowo Mbozi mkoani Songwe na ameacha mjane na watoto sita.