Nuru FM

Recent posts

12 August 2023, 10:03 am

Polisi Iringa yakamata meno ya tembo, silaha

Na Frank Leonard Oparesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, zimewezesha kukamata vipande saba vya meno ya tembo pamoja na silaha mbili zinazomilikiwa kinyume cha sheria. Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema…

12 August 2023, 8:57 am

Machinga Iringa warejea soko la Mlandege

Na Frank Leonard MKUU wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego ameunda kamati itakayoanza leo kushughulikia changamoto mbalimbali za Wamachinga, hatua inayolenga kuyapa nguvu makubaliano yanayowataka wafanyabiashara hao wadogo wa mjini Iringa kurejea katika soko lao la Mlandege. Kamati hiyo inayojumuisha…

5 August 2023, 10:25 am

Madiwani Mafinga watoa tamko bei ya nyama

Na Hafidh Ally Baraza la Madiwani halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa limeridhia bei ya nyama iuzwe kwa shilingi elfu 9 baada ya wafanyabiashara wa nyama kuuza kwa shilingi elfu 10. Hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa bei…

3 August 2023, 8:00 pm

Wazee CCM Iringa walaani wanaobeza uwekezaji wa Bandari

Na Frank Leonard Wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa wametangaza kuishiwa na uvumilivu na kuamua kulaani vikali mwenendo wenye viashiria vya kisiasa unaotishia kuigawa nchi kupitia matamko na maoni mbalimbali yanayotolewa kuhusu suala la uwekezaji wa bandari.…

31 July 2023, 2:49 pm

Ofisi za halmashauri wilaya Iringa zahamishiwa rasmi Ihemi

Na Frank Leonard Halmashauri ya wilaya ya Iringa imehamisha rasmi huduma zake za kiofisi katika majengo ya siasa ni kilimo mjini Iringa na kuzipeleka katika jengo lake jipya lililopo katika kijiji cha Ihemi, kilometa 35 kutoka mji huo, barabara kuu…

27 July 2023, 11:12 am

Kanisa la EAGT Frelimo lakemea ukatili wa kijinsia, ushoga

Na Hafidh Ally Kanisa ya EAGT Frelimo Manispaa ya Iringa limeweka mkakati wa kukemea matukio ya ukatili wa m kijinsia na ushoga kupitia ibada wanazoendesha. Akizungumza na Nuru FM Mchungaji Ezekiel Yona Mwenda kutoka Kanisa la Evangelistics Assembless of God…

26 July 2023, 7:36 pm

Mafinga wakamilisha ujenzi wa Miradi ya Boost.

Na Mwandishi wetu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Utekelezaji wa Miradi ya BOOST. Dendego ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea Shule ya Msingi Nyamalala iliyokamilisha ujenzi wa vyumba vitano(5) vya madarasa…

21 July 2023, 10:10 am

Mafinga Mji wakagua miradi ya maendeleo

Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Michael Msite imefanya ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo Halmashauri ya Mji Mafinga. Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa Shule mpya ya msingi Muungano yenye Mkondo mmoja, Ujenzi…

20 July 2023, 11:49 am

Wananchi Boma la ng’ombe wafurahia miundombinu ya barabara, zahanati

Na Hafidh Ally Wananchi wa kata ya Bomalang’ombe wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, zahanati na shule. Wakizungumza na Nuru FM baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa kwa sasa miundombinu…

15 July 2023, 11:35 am

Kakakuona aonekana Iringa Atabiri

Na Hafidh Ally Mnyama aina ya Kakakuona aliyemtabiria Mkulima Mkazi wa Kijiji cha Ihemi kupata mafanikio kupitia zao la Parachichi amekabidhiwa katika idara ya Wanyamapori Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Akizungumza wakati wa kumkabidhi Mnyama hiyo ambaye alimuokota akiwa shambani…

DIRA

Jamii yenye ustawi kielimu, kiuchumi, kiafya, kisiasa na kitamaduni.

DHAMIRA

Kuwa sauti ya jamii inayoibua kero mbalimbali kwa kushirikiana na jamii, wadau mbalimbali kuzalisha habari na vipindi kupitia vifaa na teknolojia ya kisasa na rasilimali watu yenye sifa stahiki.