Nuru FM
Nuru FM
15 April 2025, 11:50 am

Na Adelphina Kutika
Katika juhudi za kuimarisha ustawi wa vijana na kuwawezesha kiuchumi na kiafya, Shirika la SOS Children’s Villages limezindua rasmi Mradi wa Uwezeshaji wa Vijana katika Hafua za Afya ya Uzazi na Uchumi Endelevu mkoani Iringa chini ya ufadhili wa wizara ya mambo ya nje ya finland .
Akizungumza katika uzinduzi huo,Uliofanyika Katika Ukumbi wa Mkoa Iringa na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, mashirika ya kijamii, na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la SOS Tanzania, Bi Dorothy Ndege, amesema mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kupata maarifa ya afya ya uzazi, stadi za maisha, na mbinu za kujikwamua kiuchumi.

SARAFINA SANGA, ni kijana kutoka Kijiji cha Kiwele wilayani iringa na mnufaika wa miradi ya SOS, anashuhudia mabadiliko chanya katika maisha yake baada ya kupatiwa mafunzo kupitia shirika hilo.
Kwa upande wake, Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi Nuru Sovela, amepongeza jitihada za SOS na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na vijana katika kujenga uchumi endelevu.
Mradi huu unatarajiwa kufikia wanawake vijana mia 300 kutoka wilaya mbalimbali za mkoani Iringa, ukiwa na lengo kujikita zaidi katika kuwasaida wasichana na vijana katika kundi balehe katika ngazi binafsi na kijamii na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wasichana na wavulana.