Tanesco Iringa yahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
9 October 2024, 8:52 pm
Na Adelphina Kutika
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kama vyanzo vya nishati.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Iringa Bi. Grace Ntungi Katika mkutano wa wateja wa kubwa wa mkoa Iringa pamoja na Utoaji tuzo kwa wateja waliochangia pato katika shirika ,Uliofanyika katika ukumbi wa Royal Palm Manispaa ya Iringa , ambapo amesema mkakati wa Tanesco kwa sasa ni kuhamasisha wananchi matumizi ya nishati safi.
Kwa upande wake Venacy Ndialundura ambaye alikuwa mgeni rasim ,Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewataka wateja hao kujenga mahusiano na tanesco katika utoaji huduma ,huku akiwahimiza matumizi ya nishati safi ili kuboresha mazingira .
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Asas Godfrey William kama mteja mkubwa amesema wanalipongeza shirika la Tanesco kuwa na ushirikano wa kutosha pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa majukumu.
Aidha, mmoja wa Wateja wakubwa waliofika kwenye Konga hilo Phina Mungai amepongeza juhudi za mheshimiwa rais kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi tofauti na kipindi cha nyuma.
Hata hivyo wateja wakubwa waliotunukiwa tuzo kwa kuchangia pato katika shirika la Tanesco ni Kampuni ya Asas kuwa mshindi wa Kwanza ,Mshindi wa Pili kiwanda cha Karatasi Mfindi na Mshindi wa tatu Saohill wa Mufindi
MWISHO