Nuru FM

Veta Iringa yahitimisha mafunzo kwa madereva zaidi 126

20 August 2024, 9:48 am

Kamanda Bukumbi akizungumza na madereva ambao wamepewa mafunzo na chuo Cha Ufundi stadi Veta. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Iringa kimehitimisha Mafunzo kwa Madereva wa Maroli 110 na Magari ya Abiria 16 ( PSV) kwa kipindi cha wiki Mbili lengo likiwa ni kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza na Madereva hao katika mtihani wa mwisho wa mafunzo hayo katika viwanja vya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Kitwiru Manispaa ya Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Madereva wanapaswa kuzingatia mafunzo waliyopewa Kwa kipindi hicho chote ili kufanya kazi Kwa weledi.

Sauti ya Kamanda

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo chuo cha Ufundi Stadi Edmund Enugu amesema licha ya Madereva wa maroli kuwa na leseni wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara kutokana na teknolojia za magari kubadilika.

Sauti ya Mratibu wa mafunzo

Msimamizi wa Mafunzo ya Muda Mrefu Veta Iringa Baltazar Kinyamaganga amewashauri wananchi kujitokeza kwa wingi kusoma kozi ya maroli kwa kuwa inatoa fursa ya ajira siku zote

Sauti ya Msimamizi

Nae Mkuu wa chuo Ufundi stadi Veta Iringa Mwalimu Pasiens Nazareth Nyoni amesema chuo kina uwezo wa kufunzisha wanafunzi wapatao mia tano lakini bado hawajafanikiwa kufikia idadi hiyo kwa mwzi mmoja ,lakini mpango uliopo kwa sasa ni kuwa na magari mawili makubwa ili kuongeza udahiri wa wanafunzi.

Sauti ya Mkuu wa Veta

Kwa upande wao Madereva waliohitimu mafunzo hayo wamesema uendeshaji wa Magari makubwa ni fursa ya upatikanaji wa ajira tofauti na gari ndogo.

Sauti ya Madereva