Mpanda FM
Mpanda FM
25 February 2026, 11:05 am
“Nilimtuma mdogo wake hakumkuta,tukaenda wote kumtafuta hadi usiku wa saa sita hatukufanikiwa kumuona basi tukafunga mlango tukalala“ Na Anna Milanzi -Katavi Kufuatia mauaji ya Irene Yosia binti mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa mtaa wa Tulieni manispaa ya Mpanda…
24 February 2026, 7:05 pm
Baadhi ya viongozi katikati ni mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Sumry. Picha na Samwel Mbugi “Tunaishukuru serikali tumepokea vifaa tiba” Na Samwel Mbugi Hospitali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imepokea vifaa tiba 46 kutoka serikali ya awamu…
24 February 2026, 1:25 pm
Picha na mtandao wa mwananchi “Tukio hili limetushtua sana na huu ni ukatili” Na Anna Mhina Wakazi wa mtaa wa Tulieni, kata ya Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, wamepatwa na mshtuko kufuatia kukutwa kwa mwili wa msichana mmoja ndani…
23 February 2026, 7:05 pm
“Hatuwezi kutengeneza miradi kama hatukusanyi mapato” Na Samwel Mbugi Baraza la madiwani halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti zaidi ya shilingi billioni 35 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Akisoma taarifa…
21 February 2026, 7:19 pm
Wanatumia vitambaa na wengine kutumia mikono pasipo kujua njia sahihi za kitaalamu kwa ajili ya kusafisha vinywa vya watoto. Na Rhoda Elias-Katavi Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza kuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya namna sahihi…
20 February 2026, 6:16 pm
“walikuwa wakikumbana na changamoto katika shughuli za kilimo, ikiwemo ukosefu wa maji ya uhakika kwa ajili ya umwagiliaji” Na Ben Gadau – Katavi Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamkulu wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi wa skimu ya umwagiliaji, wakisema…
20 February 2026, 5:44 pm
“ameomba kuharakishwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo.“ Na Ben Gadau- Katavi Diwani wa Kata ya Ibindi Mdakuni Matongo ametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi muungano…
20 February 2026, 4:42 pm
“soko hilo linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundo mbinu hali ambayo inatishia usalama wa bidhaa za wafanyabiashara hususani nyakati za usiku.“ Na John Benjamin -Katavi Wafanyabiashara wa soko kubwa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamewaombea msamaha wa…
19 February 2026, 4:06 pm
“Nilifuatwa na mtoto kwa ajili ya kwenda kumsaidia baba yake ambaye alikuwa anavuja damu na baada ya kufika nilimkuta kaka amevunjwa Mguu.” Na Samwel Mbugi- Katavi Mwanaume mmoja mwenye umri kati 40 – 45 ambaye jina lake limehifadhiwa amepigwa na…
19 February 2026, 2:22 pm
“Amepata majeraha baada ya kuchomwa kisu cha moto na mama yake mzazi kwa madai ya kuwa na tabia ya kuomba pesa kwa majirani“ Na Rhoda Elias-Katavi Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 4 ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mpanda…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
